Home Uncategorized MDOGO WAKE FRANCIS CHEKA AIBUKA, ATAJA UKWELI KUHUSU KAKA YAKE

MDOGO WAKE FRANCIS CHEKA AIBUKA, ATAJA UKWELI KUHUSU KAKA YAKE


COSMAS Cheka, mdogo wa Francis Cheka ameibuka na kukanusha taarifa zinazosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kwamba Kaka yake alikuwa miongoni mwa wahanga waliopoteza maisha kwenye ajali ya moto mkoani Morogoro.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cosmas amesema kuwa anashangazwa na taarifa hizo ambazo zinaendelea kwa kasi jambo ambalo si jema kwani Kaka yake hayupo nchini kwa sasa.

“Kaka yangu hayupo Bongo kwa sasa yupo nchini Msumbiji ambapo anaendeleza shughuli zake za biashara kama angekuwepo ningejua.

“Mara ya mwisho kuwasiliana naye ni jana ameniambia yupo salama, wale wanaosambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo wanapaswa waache kufanya hivyo,” amesema.

Jumamosi ya wiki iliyopita kulitokea maafa mkoani Morogoro ambapo lori la kubeba mafua lilipata ajali na kulipuka.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO