Home Uncategorized MTOTO ALIYEPOTEA SIKU SITA DAR APATIKANA ARUSHA

MTOTO ALIYEPOTEA SIKU SITA DAR APATIKANA ARUSHA


MTOTO ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi na awali ya Tuwapende, Daniel Evans (12) aliyepotea Agosti 10, 2019,  jijini Dar es Salaam amepatikana leo Alhamisi Agosti 15,2019 mkoani Arusha.

Baba wa mtoto huyo, Evans Rubara, amesema mtoto wake anatarajiwa kusafirishwa kesho Ijumaa Agosti 16,2019 kupelekwa Dar es Salaam.

“Sina mengi ninayoweza kueleza zaidi ya kushukuru sana juu ya kupatikana kwake, hatujui ilikuwaje lakini tutakuwa na mengi ya kusema kesho atakapofika,” amesema Rubara.

Rubara alisema mtoto wake alitoweka katika mazingira ya kutatanisha Agosti 10,2019, nyumbani kwao Bunju, Dar es Salaam huku akiaga nyumbani kuwa amekwenda kucheza.

“Siku hiyo nilikuwa nimeenda shuleni kwao Tuwapende Watoto Nursery & Primary katika kikao cha wazazi, kwa sababu yuko darasa la saba tulikuwa tukijadili namna ya kuwasaidia kazi za nyumbani ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao lakini pia kuhusu sherehe yao ya kumaliza elimu ya msingi.

“Niliporudi nyumbani majira ya saa sita mchana nilifunguliwa geti na mdogo wangu jambo ambalo si la kawaida kwani Daniel hufanya hivyo siku ambazo yuko nyumbani,” alisema.

SOMA NA HII  SIMBA YAWATAKA MASHABIKI KUZIUNGA MKONO YANGA, KMC NA AZAM FC KIMATAIFA