Imeripotiwa kuwa watuhumiwa watano wanaendelea kusakwa na polisi kwa ajili ya kuunganishwa katika kesi ya kutekwa kwa Mfanyabiashara kijana bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’.
Upande wa mashtaka wa kesi hiyo umedai kuwa bado upelelezi unaendelea kufanyika hivi sasa ili kuweza kuwapata watekaji hao.
Kwa mujibu wa wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alieleza hayo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijin Dar es Salaam kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Watekaji hao wanatajwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini na Msumbiji ambao waliweza kumteka Mo Dewji mnamo Oktoba 10, 2018 wakati akielekea mazoezini maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao ni Henrique Simbue, Daniel Bernardo, Issac Tomu na Zacarious Junior ambao ni raia wa Msumbiji.
Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Mkuu, Huruma Shaidi, aliamua kuahirisha shauri la kesi hiyo hadi Septemba 3, 2019.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.