KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho kati ya Liverpool na Arsenal Uwanja wa Anflied kiungo Alex Oxlade-Chamberlain ana uhakika wa kuendelea kudumu ndani ya kikosi hicho baada ya kuongeza kandarasi huku Naby Keita yeye bado anaendelea kupata matibabu ya misuli kurejea kwenye ubora.
Mshambuliaji wa Liverpool ambaye ni mchawi wa mabao ya usiku, Divock Origi amesema wapo tayari kwa ajili ya kuleta matokeo kwenye mchezo huo.
Kwa upande wa Arsenal, Rob Holding aliyekuwa anasumbuliwa na goti ameanza mazoezi tayari huku Emile Smith Rowe, Hector Bellerin, Kieran Tierney na Dinos Mavropanos hawana uhakika wa kucheza kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Liverpool haijawahi kunyooshwa na Arsenal kwenye jumla ya mechi nane za mashindano ambapo walishinda nne na Sare nne.
Arsenal hawana bahati na safari zao za Anflied ambapo kwenye jumla ya michezo sita, miwili ilikuwa sare na minne walipoteza.
Na jumla zimefungana mabao 22 hivyo ni Jambo la kusubiri endapo Arsenal wataanza kuonyesha makali yao ndani kesho ugenini.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.