Home Uncategorized SHIBOUB AFICHUA MBINU ZA KUWAMALIZA UD SONGO HARAKA KWA MKAPA, HANA UTANI

SHIBOUB AFICHUA MBINU ZA KUWAMALIZA UD SONGO HARAKA KWA MKAPA, HANA UTANI


Kiungo Msudan wa Simba, Sharaf Shiboub amefunguka kuwa dawa pekee ya kuwafunga wapinzani wao, UD do Songo kwenye mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa ni kuona wanapata sapoti kubwa ya mashabiki wao kwenda kuwashangilia.

Kiungo huyo kesho Jumapili atakuwa mmoja ya wachezaji ambao watakuwa na kibarua cha kupambana na Do Songo kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa suluhu nchini Msumbiji.

Katika mchezo huo Simba wanahitaji ushindi wa namna yoyote ili kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Kiungo huyo amesema kuwa ana imani kubwa ya kushinda kwenye mechi hiyo lakini morali yao itaongezeka zaidi mashabiki wao watakapokuwa wengi uwanjani hapo kwa ajili ya kuwashangilia.

“Tuna matumaini makubwa ya kushinda mechi hii kwa sababu tuko nyumbani na tumejiandaa vizuri, lakini naona kabisa kama mashabiki wetu wakiwa wengi itakuwa vizuri zaidi.

“Wakiwepo mashabiki wengi kwenye mechi hiyo kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Azam basi naamini kabisa litakuwa jambo zuri kwetu kuweza kushinda mchezo huo,” alisema Msudan huyo.

SOMA NA HII  BEKI SIMBA AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA