Uncategorized

AZAM KUANZA NA MAKALI LIGI KUU

admin August 27, 2019 11:12 am


Uongozi wa Azam FC umesema kuwa timu yao ipo tayari kwa ajili ya msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema kikosi chao kipo tayari kupambana kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu hususan kuelekea kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya KMC leo Jumanne huku akiwaomba mashabiki waendelee kuiunga mkono timu hiyo.

“Kikosi kipo tayari kwa msimu huu mpya hususan kwenye mchezo wetu wa kwanza dhidi ya KMC siku ya Jumanne.

“Lakini nichukue nafasi hii kuwaomba mashabiki waendelee kuiunga mkono timu yetu kama walivyofanya kwenye mchezo wetu dhidi ya Fasil Kenema,” alisema Popat.

PICHAZ: SIMBA WALIVYOJIFUA GYMKHANA KWA AJILI YA MECHI NA JKT TANZANIA EXCLUSIVE: BARAKA MPENJA ATAJA TIMU ANAYOSHABIKIA – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply