Ikiwa ni baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa hasira zote wanazihamishia kwenye Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.
Simba iliondolewa kwenye na UD Songo ya nchini Botswana kwenye Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungana na 1-1 kwenye mchezo wa pili wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Beira, Msumbiji ilitoka suluhu na Songo kabla ya kurejeana na kutoka sare hiyo ya bao 1-1 ambayo keshokutwa Alhamisi itakuwepo uwanjani ikicheza mchezo wake wa ligi dhidi ya JKT Tanzania.
Akizungumza na SalehJembe, Aussems alisema kuwa hasira zote anazihamishia kwenye ligi na Kombe la FA na kikubwa kuhakikisha wanachukua makombe.
“Nawaomba mashabiki kuendelea kutuunga mkono katika ligi na Kombe la FA baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Hayakuwa malengo yetu kuondolewa katika hatua hii, bahati haikuwa yetu kwani timu ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tulishindwa kuzitumia.
“Hivyo, tunarudi kwenye ligi na kikubwa mashabiki waendelee kujitokeza uwanjani kama mwanzoni kwa ajili ya kutupa sapoti ili tufanikishe malengo yetu,”alisema Aussems.