Home Uncategorized MO AZUIA TENA PRESS YA HAJI MANARA SIMBA

MO AZUIA TENA PRESS YA HAJI MANARA SIMBA


Inaelezwa kuwa Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amezuia tena kikao alichotakiwa kukifanya Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara.

Hii itakuwa mara ya pili sasa kuahirishwa kwa mkutano huo baada ya siku kadhaa nyuma Mo kumzuia Manara asiitishe kikao ambacho alipanga pia kukifanya.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema Mo amezuia kikao hicho kilichopaswa kufanyika leo saa sita mchana.

Haijajulikana Manara alipanga kusema nini pengine tunaweza kujua siku za usoni kipi alihitaji kuzungumza.

Wakati huo, kikosi cha Simba kimeshaanza maandalizi ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  MECHI TANO ZA MWISHO, ZINAIAMUA DABI YA KARIAKOO NAMNA HII