Uncategorized

ZAHERA ATUMA UJUMBE KWA MASHABIKI YANGA

admin August 28, 2019 12:22 pm


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameandaa dozi maalum kwa ajili ya Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa leo Uwanja wa Uhuru.

Zahera alisema kuwa amewaambia wachezaji wake wote kuwa mchezo wa kwanza ni muhimu kwao kushinda.

“Tunaanza rasmi ligi kwa kucheza na Ruvu Shooting siyo timu ya kubeza kwa kuwa ipo ndani ya ligi, nimewaambia wachezaji wangu ni lazima tuwape dozi maalum wapinzani wetu kujiweka kwenye mazingira bora msimu huu.

“Tuna kazi ngumu kimataifa hilo lipo wazi lakini ndani ya ligi pia ni muhimu na niliwaambia awali kwamba tunakuja kupambana kutwaa taji la ligi na safari ndiyo inaanza kwa sasa,” alisema Zahera.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema kuwa kikosi kipo salama na wanachohitaji ni pointi tatu muhimu.

KISA MATUSI NA KEJELI SABABU YA SIMBA KUTUPWA NJE CAF, MANA ARA ATOA TAMKO LIVE! YANGA VS RUVU SHOOTING, LIGI KUU VODACOM

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply