Home Uncategorized NI SALAAAM, FALCAO AWEKA REKODI MWANZA YANGA IKIENDA SARE YA 1-1 NA...

NI SALAAAM, FALCAO AWEKA REKODI MWANZA YANGA IKIENDA SARE YA 1-1 NA PAMBA


Mechi ya kirafiki baina ya Yanga na Pamba SC imemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 1-1.


Mechi hiyo kwa Yanga imekuwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United Agosti 14 mwaka huu.

Bao la Pamba limefungwa mnmao dakika ya 30 kupitia kwa Saad Kapanga kwa shuti moja kali ambalo lilimshinda nguvu kipa Ramadhan Kabwili.

Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika, Yanga walikuwa nyuma kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakionesha juhudu za kusaka bao la kusawazisha lakini jitihada zao zilikuwa zinakwama kutokana na mabeki wa Pamba kuonesha umaridadi kwenye safu ya ulinzi.

Lakini katika dakika ya 90, David Molinga ‘Falcao’ aliyekuwa aliyepata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia, alipata nafasi nzuri na kuitumia vema akifunga bao la kusawazisha.

Bao hilo kutoka kwa Falcao linakuwa la kwanza kwake tangu asajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria.
SOMA NA HII  YANGA YATOSHANA NGUVU NA MALINDI, WACHOMOA BAO DAKIKA ZA USIKU