Uncategorized

JUVENTUS KUMNYAKUA DE GEA

admin September 9, 2019 11:10 am


Klabu ya Juventus ambayo imekuwa ikifanya usajili wa kufuru kwa miezi ya hivi karibuni, inajiandaa kumsajili kipa wa Manchester United, David de Gea.

De Gea amekuwa akiwindwa na timu kadhaa kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na ubora wake langoni. Timu za Real Madrid, PSG na Barcelona zimekuwa zikitajwa mara kwa mara kuwa zinataka saini ya kipa huyo raia wa Hispania.

Hata hivyo, sasa inaonekana kuwa Juventus itakuwa na nafasi kubwa sana ya kumtwaa kwa kuwa kipa huyo bado hajasaini mkataba mpya na timu hiyo na mkataba wake unaelekea ukingoni.

Kama kipa huyo hatasaini mkataba mpya hadi Januari basi kwenye usajili mkubwa ataondoka bure.

De Gea anaaminika kuwa anataka mshahara wa zaidi ya pauni 350,000 (Sh mil 986) kwa wiki ili abaki kwenye kikosi hicho, lakini bado hawajakubaliana na Man United.

MECHI YA SIMBA NA MTIBWA YAPANGULIWA, RATIBA MPYA YATAJWA MAKONDA AMKABIDHI JUMA KASEJA MILIONI ZAKE 10 KAMA ALIVYOAHIDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply