Uncategorized

TSHISHIMBI AONDOKA YANGA

admin January 15, 2020 9:57 pm

Inaelezwa kuwa kuwa kiungo wa Yanga, Mkongomani, Papy Tshishimbi ametimkia  kwao Congo kuangalia familia yake.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Luc Eymael, alisema Papy alimuaga siku moja kabla ya kuanza nao mazoezi, kuwa anamatatizo ya kifamilia hivyo  anasafiri kwenda kuwaona jamaa zake.

Hata hivyo alisema amempa siku chache kwa kuwa hajawahi kuwa pamoja nae mazoezini tangu ameanza, hivyo anatakiwa kuwahi ili apate muda wa kumsoma vizuri.

“Nimefuatilia baadhi ya video za Yanga, Papy ni mchezaji mzuri, lakini nahitaji awahi kurudi ili afanye mazoezi na wenzake kwani  tunakazi kubwa  ambayo inatukabili mbele yetu,”alisema Eymael.

Taarifa inasema kuwa, hata hivyo Tshishimbi ameeleza kuwa familia yake kwa sasa ipo salama, hivyo anatarajia kurudi kabbla ya mchezo wao dhidi ya Azam FC.

“Sikupanga kuja nyumbani kwa  kipindi hiki lakini amenilazimu kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezon wangu, lakini nitarudi haraka  sitaki kukosa mechi ya Azam, pia sijahudhuria maoezi na kocha wetu mpya tangu ameanza,”alisema Tshishimbi.
KAGERA SUGAR YAMUIBUA HAJI MANARA KWA FUJO, ATOA TAMKO ZITO JUU YA YANGA MBABE WA YANGA AREJEA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply