Uncategorized

AZAM FC YAJIONGEZEA NGUVU ZA KUIFUATA YANGA

admin January 16, 2020 5:57 am

IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa ushindi waliopata mbele ya Lipuli ni nguvu kwao kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa Januari, 18 uwanja wa Uhuru.

Lipuli ilikubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa, jana Januari, 15.

Mabao ya ushindi kwa Azam FC yalifungwa na Idd Chilunda na Joseph Mahundi yalitosha kuipa pointi tatu timu ya Azam FC iliyo chini ya Kocha Arstica Cioaba.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 29 na kuwa nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 na Lipuli inabaki na pointi zake 25 ikiwa imecheza jumla ya mechi 17.

SVEN WA SIMBA KWENYE MTIHANI MWINGINE LEO MBELE YA MBAO FC, MBELGIJI WA YANGA AWAVAA WACHEZAJI WAKE KISA KICHAPO CHA MABAO 3-0 MBELE YA KAGERA SUGAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply