Uncategorized

MBELGIJI WA YANGA AWAVAA WACHEZAJI WAKE KISA KICHAPO CHA MABAO 3-0 MBELE YA KAGERA SUGAR

admin January 16, 2020 5:57 am

LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake walipoteza nafasi nyingi za wazi jambo lililowafanya wakakubali kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar.

Mbelgiji huyo kwa mara ya kwanza akiwa kwenye benchi la ufundi ndani ya Yanga alishuhudia timu yake ikipokea kichapo hicho kikubwa ndani ya mwaka 2020, jana Januari 15 uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa hawakuwa na nafasi ya kupoteza bali kushinda kutokana na nafasi ambazo walizitengeneza kwenye mchezo.

“Tumetengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wetu dhidi ya Kagera, umakini wa washambuliaji pamoja na wachezaji kumalizia nafasi hizo umetufanya tushindwe kupata matokeo chanya,” amesema.

Mechi hii ni ya 13 kwa Yanga ikiwa na pointi 25 kibindoni imeachwa kwa jumla ya pointi 10 na Simba iliyo kileleni ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 na leo itakuwa kazini kumenyana na Mbao FC.

AZAM FC YAJIONGEZEA NGUVU ZA KUIFUATA YANGA HIKI NDICHO KINACHOIMALIZA KMC KUSHINDWA KUPATA MATOKEO CHANYA, DAWA YAKE YAPATIKANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply