Uncategorized

BAADA YA KUKATALIWA YANGA KISA UBORA, KINACHOENDELEA KATI YA KOTEI NA KAIZER HIKI HAPA

admin January 16, 2020 9:32 pm

Kiungo mkabaji wa zamani wa Simba, James Kotei, amethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Kaizer Chiefs inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zizagae kuwa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa usiku wa kuamkia leo.

Kotei tangu ajiunge na Kaizer Chiefs msimu huu, ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, hali iliyomfanya kuamua kuvunja mkataba.

“Ni kweli mimi na Kaizer Chiefs tumefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na sasa nipo huru kujiunga na timu yoyote. Nimepokea ofa mbili lakini bado tupo kwenye mazungumzo,” alisema Kotei.
YANGA WATOKWA NA MACHOZI, INATIA HURUMA – VIDEO BOCCO ASHINDWA KUJIZUIA, AAMUA KULIIBUA TENA SUALA LA MAPINDUZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply