ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa leo ataingia uwanjani kwa tahadhari mbele ya Yanga na hesabu zake ikiwa ni kuzipata pointi tatu muhimu.
Azam FC itamenyana na Yanga leo Januari,18 Uwanja wa Taifa utakaochezwa majira ya saa 1:00 Usiku.
Cioaba ambaye anakumbukumbu ya kuifunga Lipuli kwenye mchezo wake wa hivi karibuni amesema kuwa anatambua ugumu wa kucheza na Yanga ila atapambana kupata pointi tatu.
“Ni timu kubwa ambayo nitacheza nayo ila tumejipanga kupata matokeo chanya na tunahitaji kuzipata pointi tatu muhimu kwennye mchezo wetu,” amesema.
Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 29 imecheza mechi 14 na Yanga ipo nafasi ya nane ina pointi 25 imecheza mechi 13.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.