Uncategorized

KIMEWAKA JANGWANI, YANGA WATAKA KOCHA AONDOLEWE

admin January 19, 2020 10:08 pm

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara juzi, mashabiki wengi wa Yanga wamefunguka wakiutaka uongozi wa timu hiyo uachane na kocha mpya.

Hasira za kutaka maamuzi hayo yafanyike ni kutokana na kupoteza mechi mbili mfululizo chini ya Luc Eymael.

Kabla ya kupoteza dhidi ya Azam, Yanga ilipoteza pia mechi ya nyuma yake iliyokuwa dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilifungwa kwa mabao 3-0.

Kutokana na mwendelezo wa matokeo hayo, wengi wao wamesema ni vema kazi hiyo akaendelea nayo Mkwasa sababu alianza kuirudisha timu katika morali tofauti na Luc ambaye amekuja kuanza upya.
BAADA YA KUMFANYIA UMAFIA MCHEZAJI AZAM, SONSO AIBUKA NA TAMKO YANGA CHINI YA LUC YAWEKA REKODI YA AJABU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply