Michezo Bongo

Barabara Za AFCON Mbioni Kukamilika

Vardo July 8, 2026 10:04 am

BARABARA zinazoelekea katika Mji wa AFCON uliopo Fumba, zinatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu kwani mradi huo unategemewa kufungua fursa za kiuchumi kisiwani hapa.

Wakati akifanya ziara ya kukagua miradi ya kimkakati, Makamu wa Pili wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema ujenzi wa barabara ya Mazizini hadi Fumba ya njia sita unaendelea vizuri.

“Ujenzi wa barabara hii utakamilika mwezi Desemba na itaanza kutumika rasmi kati ya Januari au Februari 2027,” amesema.

Makamu huyo, amesema kukamilika kwa barabara hizo kutarahisisha maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) itakuwa kichocheo kizuri cha ukuaji uchumi na uwekezaji Zanzibar.

Alieleza kuwa tangu kuanza kwa ujenzi huo, Fumba imeshuhudia mabadiliko makubwa ya uchumi ikiwemo kuongezeka kwa thamani ya ardhi na wananchi kunufaika na mradi huo.

Hemed amesema, kila AFCON ikikaribia ndivyo matumaini yanavyoongezeka kwa kuwa uwanja huo sio tu kivutio cha soka Afrika badala yake ni alama ya maendeleo kwa Zanzibar.

Naye, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohamed amesema wizara hiyo inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwezi Februari 2027 miundombinu yote ianze kutoa huduma.

KVZ Yajinoa Kagame Cup 2026