Uncategorized

MBELGIJI WA YANGA APEWA ONYO

admin January 22, 2020 11:08 am


Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya Tanzania (Kamati ya Saa 72) imetoa onyo kali kwa Kocha wa Yanga Luc Eymael kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa kuhusu ubaguzi wa rangi.

Vitendo hivyo alivionyesha na kuvifanya katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam FC uliochezwa Januari 18 katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Yanga ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 ambalo lilikuwa la kujifunga kwa beki wa Yanga, Ally Mtoni katika harakati za kuokoa hatari langoni.

Aidha kamati imeutaka uongozi wa Yanga kukemea na kulitolea tamko kuhusiana na kauli hizo za ubaguzi wa rangi

YANGA: TUTAREJESHA FURAHA ILIYOPOTEA LIVERPOOL YAGOMEA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply