Home Uncategorized CHAPCHAP…SPORTPESA WAMWAGA MPUNGA NAMUNGO FC

CHAPCHAP…SPORTPESA WAMWAGA MPUNGA NAMUNGO FC


Jumanne tarehe 28 Januari, 2019 Kampuni ya ubashiri ya SportPesa imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na timu ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.


Akizungumza kwa niaba ya SportPesa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Bwana Tarimba Abbas amesema nia ya SportPesa imekuwa ni kuendeleza soka la Tanzania na kuongeza ushindani miongoni mwa Timu za Ligi Kuu.


“Nadhani mnakumbuka siku zote tumekuwa tukisema SportPesa imekuja Tanzania kwa nia ya kuendeleza sekta ya mpira wa miguu, ndio maana tuliingia mikataba na vilabu vikubwa Tanzania kama Simba, Yanga na Singida United. Pia tulitoa sapoti ya kifedha na vifaa vikiwemo jez kwa timu ya Polisi Tanzania vitu ambavyo vimekuwa chachu kwa wao kuingia Ligi Kuu” amesema BwanaTarimba.


Bwana Tarimba ameongeza kwa kusema wanaimani kubwa na Namungo FC ambayo ipo nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu na ndiyo maana wameamua kuweka udhamini huo wakiamini wanaweza kufanya vizuri na kutoa upinzani msimu huu na ujao.


Mkataba wa udhamini wa SportPesa na Klabu ya Namungo FC utakuwa ni wa mwaka mmoja na utakuwa na thamani ya Shilingi milioni 120.

Kwa upande wa Namungo FC, Mwenyekiti wa timu hiyo Bwana Hassan Zidadu aliwashukuru SportPesa kwa udhamini huo na kuahidi kutumia fursa hiyo vizuri kutimiza malengo ya Wadhamini hao.


“Tunawashukuru sana SportPesa kwa kutupa fursa hii kwa timu yetu na tunatoa ahadi ya kufanya vyema ili tuchukue ubingwa wa Ligi Kuu au Kombe la Shirikisho ili tuweze kuitangaza chapa ya SportPesa kimataifa” amesema Bwana Hassan.


“Hili ni jambo la furaha kwa timu yetu kuweza kupata udhamini wa Kampuni kubwa kama SportPesa, hakuna asiyefahamu ukubwa wa Kampuni hiyo ambayo ipo kwenye udhamini na vilabu viwili vikubwa Tanzania, Simba na Yanga. Lakini pia ni wadhamini wakuu wa Klabu kubwa Uingereza Everton. Kwahiyo tunafurahi kuwa sehemu ya familia ya SportPesa” aliongeza Bwana Hassan.


Kuhusu SportPesa

SportPesa ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha na michezo na habari za burudani. Kupitia majukwaa yetu tunatoa matokeo ya mechi papo hapo na kwa nchi nyingine tunatoa huduma ya michezo ya kubashiri na ushindi kwa wateja wetu.


Sisi ni kampuni tuliyojidhatiti kutoa huduma na kuwekeza katika maendeleo ya michezo na jamii zetu. Tunatumia nguvu ya michezo kuunganisha watu kokote ulimwenguni; kuwapa wateja wetu msisimko halisi wa michezo, kuviongezea vilabu kipato na kutoa fursa kwa wanajamii.
SOMA NA HII  ALIYEWAPA TABU SIMBA APEWA DILI ARUSHA