Uncategorized

SABABU YA JKT TANZANIA KUBADILI UWANJA MBELE YA COASTAL UNION HII HAPA

admin February 4, 2020 4:39 am


MCHEZO wa leo wa Ligi Kuu Bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Coastal Union uliopaswa uchezwe kwenye Uwanja wa Isahmuyo majira ya saa 10:00 sasa ni rasmi utachezwa Uwanja wa Uhuru.

Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Jamila Mutabazi amesema kuwa sababu kubwa ya mchezo huo kuhamishiwa Uwanja wa Uhuru ni maji kujaa kwenye Uwanja wa Isahmuyo.

“Tulipaswa tucheze kwenye Uwanja wa Ishmuyo ila kwa sasa hautachezeka tena kutokana na maji kujaa eneo la kuchezea, tumeamua kuupeleka Uwanja wa Uhuru, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

JKT Tanzania mechezo wake wa mwisho ilichapwa bao 1-0na Polisi Tanzania pia Coastal Union nao walichapwa mabao 2-0 mbele ya Simba.

AZAM FC V TANZANIA PRISONS KESHO TAIFA NI MOTO NEYMAR KUIKOSA NANTES LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply