Home Uncategorized MTAALAMU WA SOKA LA KISASA YANGA ASEPA ZAKE KWAO, KILICHOFANYIKA CHATAJWA

MTAALAMU WA SOKA LA KISASA YANGA ASEPA ZAKE KWAO, KILICHOFANYIKA CHATAJWA


NGULI na mtaalam wa mfumo wa soka la kisasa, Carraca Antonio Domingoz Pinto (pichani), amefikia muafaka na Yanga na amerejea kwao kuweka mambo sawa huku mtaalam mwingine Msauzi, mambo yakinoga.

Mreno huyo, alitua nchini kufanya mazungumzo na GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, na kufikia pazuri kabla ya kurejea tena kwa mara pili kuanza kazi Jangwani.

Sasa Yanga inayoelekea kwenye mabadiliko ya kimfumo wa uendeshaji, itakuwa na Wazungu wanne. Wengine ni kocha Mbelgiji Luc Eymael, kocha wa viungo Riedoh Berdien na daktari wa misuli, Faried Cassiem wote kutoka nchini Afrika Kusini ambao wana asili ya Ulaya.

Ujio wa Faried umekuwa raha kwa wachezaji wa Yanga kutokana na umahiri wake kwenye ishu za afya ambako sasa wana uhakika wa kutatua matatizo yao kwa wakati.

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM, Mhandisi, Hersi Said, alisema; “Alikuja kwa ajili ya makubaliano na majadiliano ambayo tayari tumefikia muafaka mzuri na ndani ya siku hizi mbili haraka atarejea nchini kwa ajili ya kuanza kazi Yanga.

“Amekuja katika projekti tunayoifanya kwenye klabu yetu, hivyo kwa kuliona hilo ndio maana tukamleta mtaalam huyu mwenye uzoefu mkubwa kutoka klabu kubwa ya Benfica.

“Tunaendelea na tutaendelea kufanya vitu vingine ambavyo vipo nje ya mkataba , lengo ni kuendelea kuisaidia timu yetu ya Yanga ili kufikia levo za kimataifa kama zilivyokuwa klabu nyingine kubwa nje na ndani ya Afrika.”
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA JUMAPILI