Uncategorized

ISHU YA SIMBA KUSHINDA DAKIKA ZA USIKU, SVEN ATAJA SABABU

admin February 7, 2020 8:14 am

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wamekuwa wakishinda dakika za usiku kutokana na wachezaji wake kutokuwa makini ndani ya uwanja.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wapo nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 19 na kujikusanyia pointi 50 kibindoni.

Kwenye mechi mbele ya Namungo FC ya Lindi ambapo Simba ilishinda mabao 3-2 Meddie Kagere alifunga bao la ushindi dakika za lala salama pamoja na ule dhidi ya Polisi Tanzania ambapo Ibrahim Ajibu alifunga bao la ushindi dakika za lala salama na Simba ilishinda mabao 2-1 zote Uwanja wa Taifa.

Sven amesema:”Tumekuwa tukishindwa kumaliza mchezo mapema kutokana na wachezaji wangu kushindwa kuongeza umakini zaidi wa kutumia nafasi ambazo wanazipata, nimeligundua hilo na ninalifanyia kazi kwa ukaribu,”.

KOCHA KAGERA SUGAR ATAJA KINACHOIBEBA TIMU YAKE, AWAPA TANO WACHEZAJI YANGA: RUVU WALIBAHATISHA, WASITARAJIE KUOKOTA DODO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply