Uncategorized

AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA POLISI TANZANIA

admin February 9, 2020 10:14 am


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wanahitaji pointi tatu za Polisi Tanzania kwenye mchezo utakaochezwa Jumanne, Februari 11,2020, Uwanja wa Uhuru.

Azam FC jana imeshinda mabao 3-1 mbele ya KMC inafikisha jumla ya pointi 41 ikiwa nafasi ya pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga, amesema kuwa kila kitu kipo sawa wataendelea kupambana.

“Tunashukuru kwa kushinda mbele ya KMC, tunahitaji ushindi mbele ya Polisi Tanzania ili kuendelea mwendo wetu wetu wa kufukuzia malengo yetu ambayo tumejiwekea,” amesema. 

BECKER WA LIVERPOOL AGOMEA KULA BATA, KAZI KAMA KAWA HARMONIZE AKUSANYA KIJIJI MWANZA, AVUNJA REKODI – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply