Uncategorized

MZUNGU WA YANGA:HUYO MOLINGA MTAMUELEWA TU

admin February 14, 2020 2:37 pm

Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa uwepo wa Molinga ndani ya Yanga ni moja ya silaha kwake itakayompa ushindi kwenye mechi zake zote.

Molinga ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga akiwa na mabao 7 anafuatiwa na Patrick Sibomana mwenye mabao manne na asisti moja.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymael amesema kuwa amezungumza na Molinga kuhusu tatizo lake la kukosa utulivu jambo litakalompa nafasi ya kufunga mabao mengi na kutengeneza nafasi kwanye mashindano watakayoshiriki.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa kuwa wapinzani wetu wanazidi kujipanga hilo tunalitambua na tunalifanyia kazi na kwa uwezo ambao anauonyesha Molinga atafunga mabao mengi, jambo litakalofanya mashabiki wafurahi” alisema.

Yanga imefunga jumla ya mabao 24 ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 ipo nafasi ya tatu na pointi zake 38 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Tanzania Prisons.
NAMUNGO FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MWADUI FC MEDDIE KAGERE AKWAMA DAKIKA 360 BILA KUTUPIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply