Uncategorized

SIMBA YAOMBA SAPOTI KUTOKA KWA MASHABIKI

admin February 18, 2020 10:52 am

NAHODHA wa Simba, John Bocco amewaomba mashabiki wa Simba kuendelea kuwapa sapoti wachezaji wakiwa wanacheza nao watapambana kufikia malengo waliyojiwekea.

Bocco ana mabao matatu ndani ya ligi na pasi moja ya bao kwenye jumla ya mabao 46 ya Simba.

Simba leo itakuwa na kibarua mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 3-0 mchezo wa kwanza uliochezwa Kaitaba.

Bocco amesema:”Mashabiki tunawashukuru kwa kuwa wamekuwa nasi bega kwa bega ila tunaomba waendelee kutupa sapoti kwenye kila mechi ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea,”.

Simba inaongoza ligi ikiwa na jumla ya pointi 56 kibindoni inafuatiwa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na ina pointi 44.

BIASHARA UNITED KUMALIZANA NA JKT TANZANIA LEO SABABU ZA MAKOCHA MBAO FC KUBWAGA MANYANGA HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply