Home Uncategorized KAGERA SUGAR YATAJA KILICHOWAKWAMISHA MBELE YA SIMBA

KAGERA SUGAR YATAJA KILICHOWAKWAMISHA MBELE YA SIMBA


JUMA Nyosso, nahodha wa Kagera Sugar amesema kuwa wapinzani wao Simba walitumia kosa moja walilofanya kuwaadhibu kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Jana Februari 18, Kagera Sugar ilikubali kufungwa bao 1-0 mbele ya Simba mchezo wa pili wa mzunguko wa pili ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza ule wa kwanza Kaitaba kwa kufungwa mabao 3-0.

“Tulipambana mwanzo mwisho na tulistahili pia kupata matokeo ila bahati haikuwa yetu, wametumia kosa letu moja wakapata matokeo nasi tunajipanga kwa ajili ya mechi zinazofuata, mashabiki watupe sapoti,”.

Bao pekee la ushindi kwa Simba lilipatikana dakika ya 60 kwa mkwaju wa penalti aliofunga Meddie Kagere baada ya nahodha John Bocco kuchezewa faulo ndani ya eneo la 18 na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti.

SOMA NA HII  HAPA NDIPO AMBAPO GARI LA AZAM FC LITAPAKI KUSEPA NA WACHEZAJI HAWA