HARUNA Harerimana, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakisahau maelekezo wanayopewa wanapoingia uwanjani jambo linalomfanya ashindwe kupata matokeo.
KMC ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Namungo FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Februari 18.
“Wachezaji wangu ninawapa maelekezo ya kufanya kipindi cha kwanza tatizo wakiingia uwanjani wanasahau na kufanya mambo mengine, jambo hilo linanilafanya nikirudi mapumziko kuanza upya.
“Tukiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ninaanza tena upya kuwafundisha kwa kuwa yale niliyowafundisha mwanzo wanasahau,” amesema.
KMC ipo nafasi ya 17 na pointi 21 imecheza mechi 23 ndani ya ligi.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.