Uncategorized

PAMOJA NA KUMCHAKAZA WILDER KWA TKO, FURRY ALIKUWA AMEONGOZA RAUNDI ZOTE SABA KWA POINTI

admin February 23, 2020 1:11 pm



Tyson Fury amentwanga Deontay Wilder kwa TKO katika raundi ya saba baada ya kocha wa bondia huyo Mmarekani kulazimika kutupa taulo ulingoni.

Pamoja na kumchapa Wilder, Furry anayetokea nchini Uingereza imeonyeshwa aliongoza kwa raundi zote saba, hivyo alikuwa na nafasi ya kushinda kwa pointi pia.

Muda mwingi wa pambano hilo, Wilder aliyekuwa hajawahi kupoteza alikuwa akipokea makonde makali na raundi ya pili aliumia sikio watangazaji wakieleza alipasuliwa ngoma ya sikio.

Kwa sasa Furry maarufu kama The Gypsy amekamilisha kubeba mikanda yote mikubwa ya uzito wa juu akichukua huo wa WBC kutoka kwa Wilder. Kabla alikuwa na mikanda ya WBA, WBO, IBF na IBO ambao aliutwaa akimshinda Wladimir Klitschko.

LEO BALAA MECHI KAMA ZOTE, UNITED, PSG UWANJANI, BONGO PIA YANGA, ALLLIANCE KAZINI, RATIBA HII HAPA MSIMAMO WA AZAM FC HUU HAPA NDANI YA LIGI KUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply