JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa walitambua uimara wa wapinzani wao Yanga jambo lililowafanya wapambane kutafuta matokeo licha ya kuambulia sare ya bila kufungana.
Coastal Union ilikaza mbele ya Yanga, jana Februari 23 kwa kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao wanaoongozwa na nyota wao Bernard Morrison raia wa Ghana.
“Tulitambua mchezo wetu utakuwa mgumu ukizingatia kwamba wapinzani wetu walitoka kupata sare nasi tulitoka kupoteza makosa yetu tuliyafanyaia kazi, nawapongeza wachezaji katika hilo,”.
Coastal Union imeambulia pointi moja mbele ya Yanga, kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Yanga ilishinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu jumla.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.