Habari za Michezo leo
Uncategorized

ALLIANCE: HATUNA UJANJA WA KUPENYA ROBO FAINALI BALI NI BAHATI TU

admin February 27, 2020 1:44 am


FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Alliance FC amesema kuwa ushindi wao walioupata mbele ya JKT Tanzania sio ujanja bali ni bahati kwani penalti hazina mwenyewe.

Minziro alikiongza kikosi chake kwenye ushindi wa panalti 5-3 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora wa Kombe la Shirikisho.

Dakika tisini zilikamilika kwa timu hizo kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1.

Minziro amesema:”Haikuwa kazi nyepesi na wala sio ujanja wangu kwani wapinzani wetu walipambana na mwisho wa siku penalti hazina mwenyewe nasi tumepita.

“Tutakwenda kupambana hatua inayofuata kwani tunatambua kwamba ushindani mbele ni mkubwa kuliko wakati wa sasa,” amesema.

MZUNGU WA SIMBA HALAZI KIKOSI CHAKE, LEO KAZI INAANZA RASMI KOCHA MPYA LIPULI ABEBA MATUMAINI MAPYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply