KOCHA Mkuu wa Lipuli Nzeyimana Mailo raia wa Burundi amesema kuwa ana imani ataleta mabadiliko ndani ya timu ya Lipuli baada ya kupewa kandarasi ya mwaka mmoja kutokana na kuiona timu kwenye mechi tatu.
Mailo alikuwepo kwenye jukwaa wakati Lipuli ikicheza na Simba, Mbeya City na Tanzania Prisons aikuwa akiifundisha timu ya Framboo ya Burundi amechukua nafasi ya Mrundi mwenzake Harerimana Haruna ambaye yupo na KMC.
“Timu haipo kwenye nafasi nzuri ila kwa muda ambao nimeiona timu nina imani kwamba kuna mambo yatabadilika na timu itapata matokeo, kuhusu kupoteza mechi zake ni sehemu ya mpira kwani hata timu kubwa zinapoteza,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.