Uncategorized

GWAMBINA: YANGA WALITIBUA MIPANGO YETU KIPINDI CHA KWANZA

admin February 27, 2020 2:14 pm


FULGENCE Novatus, Kocha Mkuu wa Gwambina FC amesema kuwa wapinzani wao Yanga waliwazidi mbinu dakika 45 za mwanzo na kutibua mpango wao waliojiwekea mapema kabla ya mchezo.

Gwambina jana, Februari 26 ilikubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Yanga mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho na kufungashiwa virago jumlajumla.

“Tulipanga ndani ya dakika 15 za mwanzo tupate ushindi na zile dakika 15 zinazofuta tufunge bao jingine ila zile za mwisho 10 ilikuwa tulinde sasa wao wakashinda kwenye dakika zetu 10 ambazo tulizigawa kwa hesabu hizo.

“Baada ya kufungwa walitibua mipango yetu ndio maana tukarudi kulinda na kushambulia kwa kushtukiza ila sio mbaya kwa kuwa tumetolewa tunakwenda kujipanga kwenye Ligi Daraja la Kwanza,” amesema.

SIMBA:HAKUNA KOMBE GUMU KAMA SHIRIKISHO AZAM FC YATAJA SABABU YA KUPIGIANA MIKWAJU NA IHEFU, SOKOINE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply