Uncategorized

KOCHA MPYA LIPULI ABEBA MATUMAINI MAPYA

admin February 27, 2020 4:14 am


 KOCHA Mkuu wa Lipuli Nzeyimana Mailo raia wa Burundi amesema kuwa ana imani ataleta mabadiliko ndani ya timu ya Lipuli baada ya kupewa kandarasi ya mwaka mmoja kutokana na kuiona timu kwenye mechi tatu.

Mailo alikuwepo kwenye jukwaa wakati Lipuli ikicheza na Simba, Mbeya City na Tanzania Prisons aikuwa akiifundisha timu ya Framboo ya Burundi amechukua nafasi ya Mrundi mwenzake Harerimana Haruna ambaye yupo na KMC.

“Timu haipo kwenye nafasi nzuri ila kwa muda ambao nimeiona timu nina imani kwamba kuna mambo yatabadilika na timu itapata matokeo, kuhusu kupoteza mechi zake ni sehemu ya mpira kwani hata timu kubwa zinapoteza,” amesema.


ALLIANCE: HATUNA UJANJA WA KUPENYA ROBO FAINALI BALI NI BAHATI TU HIZI HAPA ZILIZOFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply