Uncategorized

KOCHA KMC MGUU NJE MGUU NDANI, HOFU YA KUPIGWA CHINI YATAWALA

admin February 28, 2020 4:18 am


HARERIMANA Haruna, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kwa sasa anahofia kibarua chake kuota nyasi kutokana na mwenendo wa timu yake ulivyo ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na kupigwa chini kwenye Kombe la Shirikisho.

KMC ilitolewa na Kagera Sugar kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penalti 2-0 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu.

Kwenye Ligi Kuu Bara KMC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 24.

“Wachezaji wamekuwa hawanielewi kile ambacho ninawaambia kipindi cha kwanza wanafanya vitu vya kitofauti wanavyovijua wao jambo linalonifanya kipindi cha mapumziko nianze kuwaelekeza upya, nina mashaka huenda mambo yatakuwa magumu ndani ya KMC hasa kwa upande wa nafasi yangu,” amesema.

Harerimana alitua KMC akitokea timu ya Lipuli FC ambapo alidai kuwa hakulipwa stahiki zake kwa muda mrefu.

MKWASA AKABIDHIWA MIKOBA YANGA, NI NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA ISHU YA WACHEZAJI WA YANGA KUCHIMBISHWA KWENYE VYUMBA VYAO IPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply