Uncategorized

YANGA: GWAMBINA WANARUDI MWANZA KUCHEZA NGOMA

admin February 28, 2020 7:18 am

HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kutinga kwao hatua ya robo fainali mbele ya Gwambina kunawapa muda wapinzani wao kurejea Mwanza kuendelea na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kucheza ngoma.

Februari 26 Yanga ilitinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Gwambian FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Haruna Niyonzima dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa nye ya 18.

Bumbuli amesema:-“Hatukuwa na matokeo mazuri ila tulipambana na kupata ushindi mbele ya Gwambina, kwa ushindi huo inatoa fursa ya kusonga mbele huku wapinzani wetu Gwambina wao wakirudi kwenye Ligi Daraja la Kwanza na kuendelea na utamaduni wao wa kucheza ngoma kama ambavyo tuliwaona,”.

AUBAMEYANG AKOSA FURAHA KISA KUKOSA KUTINGA HATUA YA 16 BORA EUROPA SIMBA: HAKUNA MUDA WA KUPUMZIKA, KAZI JUU YA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply