Home Uncategorized ALLIANCE WATAJA KILICHOWAPONZA WAKACHAPWA MABAO 2-0 MBELE YA YANGA

ALLIANCE WATAJA KILICHOWAPONZA WAKACHAPWA MABAO 2-0 MBELE YA YANGA


GEOFREY Luseke, beki wa timu ya Alliance amesema kuwa hawakustahili kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wapinzani wao Yanga.

Jana, Februari 29, Alliance ya Mwanza ilikubali kichapo kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Luseke amesema:’Haikuwa mipango yetu kupoteza mbele ya wapinzani wetu Yanga ila kutokana na wao kutumia makosa yetu basi wameweza kutushinda kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zinazokuja,” .

Alliance FC ipo nafasi ya 13 imejikusanyia pointi 29 kibindoni baada ya kucheza mechi 25.

SOMA NA HII  SIMBA YAPIGWA KIDUDE KIMOJA CHA NYUMBANI, NJE KIMATAIFA KUISHABIKIA YANGA NA AZAM FC