Uncategorized

JKT TANZANIA: TUPO TAYARI KUVAANA NA AZAM FC, SAPOTI YA MASHABIKI

admin February 29, 2020 6:18 am


ABDALAH Mohamed,’Bares’, Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa leo vijana wake watapambana mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri.

Azam FC imeshatia timu mkoani Dodoma, leo itakuwa na kazi ya kumenyana na JKT Tanzania mchezo wake wa tatu ikiwa ugenini.

Bares amesema:”Kikosi kipo tayari na kila mchezaji amepewa majukumu yake ya kufanya, sapoti ya mashabiki inahitajika,”.

Azam FC ilitoka kumalizana na Ndanda na Namungo, nyanda za juu kusini na iliambulia pointi moja na kupoteza nne kati ya sita baada ya kupata sare moja na Ndanda kisha ikachapwa na Namungo FC bao 1-0.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI UJUMBE HUU WA ALLIANCE WATUMWA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply