Uncategorized

KOSA KUBWA LA MTIBWA SUGAR KUMBE ILIKUWA KUZITUNGUA SIMBA NA YANGA

admin February 29, 2020 3:48 pm

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kosa lao kubwa ilikuwa kuzifunga Simba na Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi jambo lililowafanya wakamiwe na timu nyingine wanapocheza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa timu nyingi zimeanza kuwapigia hesabu kali kwa kucheza nao kwa kukamia jambo linalowapa matokeo mabovu.

“Tuliposhinda Kombe la Mapnduzi kwa kuwafunga vigogo Simba na Yanga hapo ndipo matatizo yalipoanzia, timu nyingi zilianza kucheza nasi kwa kutukamia jambo lililofanya mechi zetu zote kuwa ngumu.

“Wachezaji nao walikuwa na kazi ya kufanya ila walishindwa kupata matokeo mazuri, ni mbaya kwetu na inaumiza ila tutapambana kurejea kwenye ubora wetu,” amesema. 

Mtibwa Sugar ilitwaa taji la Mapinduzi kwa kuifunga Simba bao 1-0 kwenye fainali na ilitinga hatua ya fainali kwa kuinyoosha Yanga kwa mikwaju 3-2 ya penalti baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA KMC YANGA YAFUTA BUNDI LA SARE, LAICHAPA ALLIANCE MABAO 2-0 UWANJA WA TAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply