Home Uncategorized WAAMUZI WAJITOA LIGI KUU BARA

WAAMUZI WAJITOA LIGI KUU BARA


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limepokea maombi ya waamuzi saba wanaotaka kutopangwa kuchezesha baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara kutokana na presha na uoga wa kuboronga katika kufanya maamuzi.

Ishu hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya sakata la waamuzi kuboronga katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara zilizochezwa hivi karibuni huku baadhi yao wao wakikumbana na adhabu.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, amesema wamepokea maombi hayo, lakini wakaona hilo siyo suluhisho la kuondoa tatizo na badala yake wana mpango wa kuwaandalia kozi maalumu itakayowanoa na kuwafanya wawe bora katika siku za usoni.

Kidao ameliambia Spoti Xtra kuwa, watawapima waamuzi wote kujua kama wana matatizo ya kiafya kwani kuna uwezekano wakawa na matatizo ya kutoona mbali.

“Tumepokea barua za waamuzi saba wakiomba kutopangwa katika michezo ya ligi, hiyo inatokana na presha na hofu waliyonayo, lakini kutokana na maazimio yaliyotolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia, tumeamua kuanzisha program maalumu ya kuwajengea uwezo wa ndani na nje ya nchi waamuzi wote, ambapo tutawapima afya, ikiwa kuwachunguza kama watakuwa na matatizo ya kutoona mbali.

“Lakini pia tutawachunguza wakufunzi wao ili kuona kama uwezo wao unakidhi kiwango cha kuwafanya waamuzi wetu wawe bora zaidi, lakini pia tutaunda kamati ya kuwachunguza waamuzi wote kila mara ili kubaini maendeleo yao, hii itakuja mara baada ya kuwaongezea ujuzi,” alisema Kidao ambaye ni mchezaji wa zamani wa Vijana ya Ilala.

Kwa upande wa uwepo wa madai ya waamuzi hao, Kidao alisema: “Kweli tunadaiwa, lakini tunadaiwa michezo ya raundi saba kati ya zile 19 hadi 20 ambazo timu zimecheza, lakini suluhisho la hili, tupo katika mikakati ya kupata wadhamini ambao watakuwa wanashughulikia malipo yao tu.

“Kwa msimu mmoja, waamuzi wa Ligi Kuu Bara, wanalipwa zaidi ya Sh bilioni moja, ambapo wadhamini wetu wanatoa Sh milioni 426 kama fedha za malipo kwa waamuzi, fedha inayobaki ambayo ni zaidi ya Sh milioni 600, zinalipwa na TFF, Kwa hiyo tunataka kuepusha hili kwa kutafuta wadhamini wao
SOMA NA HII  YANGA KUIPELEKA BODI YA LIGI FIFA