Uncategorized
KIONGOZI MPYA WA AZAM FC HUYU HAPA, ARITHI MIKOBA YA MAGANGA
UONGOZI wa Azam FC unayofuraha kumtangaza mwandishi mkongwe, Thabith Zakaria ‘Zaka Za Kazi’, kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
Zakaria anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaffar Idd, aliyepangiwa majukumu mengine ndani ya kampuni.
Ujio wa Zakaria ni sehemu ya jitihada za uongozi wa Azam FC kuboresha kitengo cha habari ndani ya timu, ambapo sasa kitatambulika kama Kitengo cha Habari na Mawasiliano kitakachokuwa kikiongozwa naye.
Tunaamini ya kuwa Zakaria atatumia vilivyo uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika tasnia ya habari, alioupata wakati akifanya kazi na makampuni makubwa ya habari ya IPP Media na Azam TV, na kuitangaza vema timu yetu.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.