PASCAL Wawa, beki wa Simba amesema kuwa kinachowafanya waendelee kupata matokeo ndani ya Uwanja ni ushirikiano pamoja na mtazamo wa kutazama mambo yanayofuata.
Simba ikiwa imecheza mechi 26 inaongoza ligi ikiwa na pointi 68 na jana Machi 4, ilishinda mchezo wao mbele ya Azam FC kabla ya kukutana na Yanga Machi 8 Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa kila baada ya mechi huwa wanatazama kazi inayofuata jambo linalowapa nafasi ya kupata matokeo.
“Kila baada ya mechi kumalizika tunaanza kutazama yale yajayo tunasema ‘focus’ sasa hii inatupa nguvu ya kujua wapi tulikosea na nini tukifanye, kikubwa pia kinatusaidia ni ushirikiano uliopo,”.
Wawa kwenye mchezo wake dhidi ya Azam FC alikuwa mchezaji pekee wa Simba aliyeonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo mchezaji wa Azam FC.