Uncategorized

MUSONYE ASEPA CECAFA BAADA YA KUDUMU MIAKA 21, MRITHI WAKE HUYU HAPA

admin March 11, 2020 12:24 pm
WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Soka kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa Rais wa CAF Ahmad Ahmad amethibitisha jina la Auka Geucho na kulipitisha ili awe Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA.

Geucho raia wa Kenya amechukua mikoba ya Nicolas Musonye aliyekuwa Katibu Mkuu wa CECAFA kwa muda wa miaka 21 kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza muda kutokana na utendaji wake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Karia amesema kuwa wanathamini mchango wa  Nicolas Musonye ambaye amekaa madarakani kwa muda mrefu na wanaamini wataendelea kushirikiana katika kazi za kuendeleza soka la Afrika Mashariki na Kati.

“Tumefanya naye kazi kwa ukaribu na amekuwa akitoa ushirikiano kwa kuwa nafasi yake amepatikana kiongozi mwingine bado ataendelea kuwa kwenye familia yetu ya mpira na kila kitu kitakwenda sawa.

 Musonye amesema kuwa kwa muda wa miaka 21 aliyofanya kazi ametimiza mambp mengi ya mafanikio licha ya chokochoko nyingi na anafurahi kufanya kazi na watanzania pamoja na Serikali ya Tanzania kiujumla.
REKODI ZAIBEBA SIMBA LEO UWANJA WA TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA SINGIDA UNITED, LUIS NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply