Home Uncategorized YANGA:TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KMC

YANGA:TUNAZITAKA POINTI TATU ZA KMC


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa leo utapambana kupata pointi tatu mbele ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa majira ya saa 10:00 Uwanja wa Taifa.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa maandalizi yamekamilika kilichobaki ni suala la muda tu wa kuonyesha uwezo wao.

“Haitakuwa kazi nyepesi ila tumejipanga kuona namna gani tunaibuka na ushindi na kupata pointi tatu, kwa sasa kila mchezaji anatambua kazi yake nina imani tutafanya vizuri,” amesema.

Yanga itashuka uwanja wa Taifa ikiwa na kumbukumbu ya kuichapa bao 1-0 Simba kwenye mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Machi 8,2020.

SOMA NA HII  BALAA LA KAKOLANYA LIPO NAMNA HII UWANJANI