Uncategorized

HUYU HAPA ATAJWA KUWA NYUMA YA UBORA WA MARTIAL WA MANCHESTER UNITED

admin March 12, 2020 1:24 am


IMEELZWA kuwa ubora wa Anthony Martial ndani ya Manchester United unazidi kuimarika tofauti na awali kutokana na ujio wa nyota mpya ndani ya kikosi hicho.

Gwiji wa Klabu ya Manchester United, Roy Keane amesema kuwa ubora wake unatokana na ujio wa mshambuliaji mpya, Odion Ighalo.

Ighalo alijiunga na United ili awe mbadala wa Rashford ambaye ni majeruhi akitokea Klabu ya Shanghai Shenhua ya China kwa mkopo na ametupia mabao matatu.

Keane amesema ujio wa Ighalo umeongeza umakini na utulivu kwa Matial ambaye amepata mpinzani wake.


 “Muda mwingine mshambuliaji anapokuja mnampa pongezi na anawainua wengine akipambana, Martial amejibu baada ya kufikiri kwamba amepata mchezaji mwingine wa kupambania namba hili ni jema,” amesema.

MRITHI WA MUSONYE ATOA YAKE YA MOYONI NDANI YA CECAFA NAHODHA WA REAL MADRID AWATAKA WACHEZAJI KUJIKOSOA ILI KUTWAA UBINGWA WA LA LIGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply