NYOTA wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya asijiunge na kikosi cha Yanga ambacho leo kitacheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC ni kadi zake tatu za njano alizopewa kwenye mechi alizocheza.
Niyonzima amesema kuwa hajagoma kuendelea kuitumikia n Yanga kama ambavyo inaelezwa kwani yeye ni mali ya Yanga.
“Inaelezwa kuwa nimegoma kuitumikia timu yangu hiyo sio kweli bado ni mali ya Yanga ila nimeshindwa kujiunga na wenzangu kutokana na kuwa na kadi tatu za njano,” amesema.
Niyonzima amekuwa akitimiza majukumu yake ndani ya Yanga ambapo kwenye mechi zote mbili dhidi ya mabosi wake wa zamani Simba alionyesha balaa lake ndani ya dakika zote 180.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.