Uncategorized

SABABU YA MBELGIJI KUMRUDISHA AJIBU SIMBA B, HIZI HAPA….

admin March 16, 2020 7:22 am


Kutokana na kutokuwa na uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ibarahim Ajibu, pamoja na wenzake wasiokuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza, Ijumaa ijayo wanatarajiwa kupelekwa Simba B.

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amewaandalia wachezaji hao mechi ya kirafiki na Simba B ambayo watacheza kwa ajili ya kuongeza viwango vyao katika kipindi hiki ambacho michuano ya Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa.

Sven alisema kuwa mchezo huo ni moja ya mikakati yake ya kuhakikisha wachezaji wote ambao hawana nafasi katika kikosi chake cha kwanza wanautumia katika kuongeza uwezo wao.

β€œLicha ya ligi kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa, sisi tunaendelea kujifua kama kawaida.

β€œTunafanya mazoezi ya nguvu ambayo yanalenga kabisa kuwaweka sawa wachezaji wote ili waweze kuwa fiti na zaidi ni wale ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza.

β€œKwa hiyo, siku ya Ijumaa tutakuwa na mechi ya kirafiki na Simba B, wachezaji ambao watapambana na timu hiyo zaidi watakuwa ni wale ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza,” alisema Sven.

SOURCE: CHAMPIONI
NAKUKUMBUSHA WAZIRI LUKUVI, MIUNDOMBINU IELEKEE KWA KINA SAMATTA WAPYA NAMUNGO YATAJA KINACHOWABEBA WAKIWA NDANI YA UWANJA WA MAJALIWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply