TIMU ya Mtibwa Sugar ambayo leo ilikuwa ina mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Mkwakwani inatarajia kuanza safari ya kurejea Morogoro leo kutokana na ligi kusimamishwa.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kwa sasa wanajiandaa ili kuanza safari kurejea Morogoro baada ya ligi kusimamishwa.
“Tumepokea taarifa kuhusu kusimamishwa kwa Ligi Kuu Bara kutokana na kupambana na ugonjwa wa virusi vya Corona hivyo hatupingi tunatekeleza agizo bila hiyana na tunawaomba watanzania wachukue tahadhari,” amesema.