BEKI wa Kulia wa Yanga amesema kuwa kitendo cha timu yake kuruhusu mabao kwenye mechi zao mbili ni hatari kwa afya ya timu yao kutokana na makubaliano ambayo waliyaweka kwa pamoja ndani ya timu.
Yanga iliyo chini ya Luc Eymael imeambulia pointi moja kwenye mechi mbili ilizocheza sawa na dakika 180 baada ya kuibamiza Simba bao 1-0 Uwanja wa Taifa Machi 8.
Machi 12 ilifungwa bao 1-0 na KMC Uwanja wa Uhuru kisha ikalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC Machi 15 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.
Abdul alisema kuwa walikubaliana tangu mwanzo kucheza kwa umakini na kutoruhusu mabao kupenya kwenye ngome yao jambo ambalo limetokea kwenye mechi zao.
“Wachezaji tulikubaliana kutimiza majukumu yetu ili tusifungwe kwa kuwa imetokea ni wakati mwingine tena kuzungumza pale tulipokesa na kocha atatupa maelekezo yake tutayafanyia kazi kwani matokeo mabaya hatuyafurahii,” amesema.
Yanga ikiwa imecheza mechi 27 ikiwa nafasi ya tatu imefungwa mabao 20 na ina pointi 51 kibindoni huku mpinzani wake Simba akiwa nafasi ya kwanza na pointi 71.
Mabao ya kwenye mchezo yote mawili yalifungwa kwa kichwa ambapo Tariq Seif alianza kuandika bao kipindi cha kwanza kwa pasi ya Abdul na Bigirimana Blaise alifunga kwa pasi ya Lukas Kikoti.
Bernard Morrison kiungo mshambuliaji ambaye aliukosa mchezo mbele ya KMC kutokana na kusumbuliwa na majeraha alirejea uwanjani na kufanya yake wakati timu yake ikisepa na pointi moja ugenini.
Thanks , I’ve just been searching for info about this topic for
a long time and yours is the greatest I have discovered till
now. But, what concerning the conclusion? Are you certain in regards to
the source?
my site Food packaging
Your articles are so easy to understand, thanks. Regards, IDProperti.com | Pasang Iklan Properti
Hello from Happykiddi.