MTENDAJI Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin Amesema kuwa marekebisho ya Uwanja wao wa Azam Complex yamechangia kwa kiasi chake kuiweka timu hiyo nafasi ya pili kutokana na kutoutumia kwa muda mrefu uwanja wao waliouzoea.
Marekebisho ya Uwanja huo yalianza Desemba,2019 kwa kufanyia maboresho sehemu ya kuchezea na kwa sasa yamefika hatua nzuri.
“Maboresho ya uwanja wetu wa nyumbani kwa kiasi chake yamechangia kuongeza ugumu wa kupata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tulicheza kwani tungetumia uwanja wetu isingekuwa rahisi kupoteza tungekuwa nafasi ya kwanza,” amesema.
Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 28 kibindoni ina pointi 54 kwa sasa imevunja kambi yake mpaka Aprili 17.